HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 24, 2014

RAIS KIKWETE AHUDHURIA SHEREHE ZA KULA KIAPO ZA RAIS ZUMA WA AFRIKA KUSINI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini leo Mei 24, 2014.
Rais Jacob Zuma akila kiapo katika Nelson Mandela Amphitheater katika jengo la Union Buildings mjini Pretoria wakati wa sherehe za kuapishwa kwake leo Mei 24, 2014. 
Ndege za kijeshi zikiunda umbo la "20" kuashiria miaka ishirini ya uhuru kamili wa Afrika Kusini katika sherehe za kuapa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014.
Marais na viongozi toka nchi mbalimbali wakiondoka Union Buildings baada ya kushuhudia Rais Jacob Zuma akiapa kuwa Rais wa Afrika Kusini kwenye ukumbi wa wazi wa Mandela katika jingo la Union Buildings mjini Pretoria, Afrika Kusini, leo Mei 24, 2014  PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad