HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 1, 2014

PPF ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI LEO,RAIS KIKWETE AKAMKABIDHI ZAWADI MFANYAKAZI BORA WA PPF

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 5, mfanyakazi bora wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Herman Kachima, wakati wan kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa zilifanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau (Wapili kulia), akiteta jambo na mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio, na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii, (SSRA), Irine Isaka (Kushoto), na mwenyekitinwa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (Juu), wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimsalimia mjumbe wa bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaraka Igangula, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita kwenye maandamano mbele ya mgeni rasmi, rais Jakaya Kikwete (Hayupo pichani) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (Kushoto), akimsikiliza kwa makini, Naibu Katibu mMkuu wa Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Profesa Ole Gabriel, wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad