HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 31, 2014

MUONGOZA FILAMU MAARUFU NCHINI,GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA USIKU HUU KUTOKA MKOANI MOROGORO ,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA KUTOKANA NA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM,WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW,KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA KWA MIPIRA MIWILI (MATAIRI) YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH.

AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.

NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU NANE,KATI YAO NI WAPIGA PICHA WA SHOW HIYO AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad