· Watanzania Marekani wametoa dolla 5,300
· Familia, ndugu na Jamaa wa Tanzania wametoa dolla 11,000
· Watoto wa Marehemu Erick na Mary Kagaruki wametoa kiasi kilichobakia cha dolla 3,700.
Watoto wa Marehemu Erick Kagaruki na Mary Kagaruki na familia nzima ya Marehemu mama Harriette Peace Kagaruki wanapenda kuwashukuru wote mliotoa michango, rambirambi na mliofanikisha kwa namna moja au nyingine shughuli hizi za msiba ziweze kufanikiwa.
Shukrani nyingine ziende kwa Watanzania wote na rafiki wa Watanzania waliochangia shughuli za msiba huu hapa Marekani na Tanzania.
Mwili wa Marehemu umeshaletwa New Jersey kutoka Philadelphia tayari kupelekwa Tanzania siku ya Jumanne usiku saa tatu kupitia airport ya Newark na British Airways via Entebbe.
Mwili utawasili Entebbe Jumatano kabla ya safari ya kuelekea Bukoba kuanza kwa ajili ya shughuli mazishi kuanza.
Familia inapenda tena kuwashukuru wote kwa kufanikisha michango na shughuli za sasa za msiba huu. Tunawaomba Watanzania wote tuendelee kushirikiana katika nyakati za shida na raha kama tulivyoshirikiana wakati huu wa msiba.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Byabusha – 914-584-7502
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
Deogratius Mhella,
Katibu New York Tanzanian Community.
No comments:
Post a Comment