Abiria
wanaotumia njia ya makumbusho kuelekea Mwenge wakitokea Tandika na
Mbagala leo wameonja Joto ya jiwe kwa takribani masaa manne baada ya
mabasi yanayoptumia kituo cha ndani kugoma kupeleka abiria mwenge
kutokana na ubovu wa barabara za ndani wanazotumia kupita kuelekea kituo
cha mwenge.
Sakata
hilo lilianza pale magari yalipofika kituo cha ndani cha makumbusho na
kuwashusha abiria wote na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea
mwenge,ndipo mzozo mkubwa ulipozuka na kupelekea Sumatra na vyombo vya
Usalama kufika eneo La Tukio na kuweza kuongea na madereva hao,lakini
madereva hao na makondakta waliendelea kugoma mpaka pale walipohaidiwa
kuwa ndani ya wiki moja barabara hizo zitakuwa zimerekebishwa na kuwa
nzuri,hivyo watumie njia kuu kuelekea mwenge.
Kamanda wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho kuelekea mwenge.
Hapo
ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata
mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo
kuendelea na safari.
Hili
ni moja ya basi la abiria likiwa limewekea magogo ili lisiweze
kuendelea na safari kuelekea mwenge Bali kuishia kituo cha makumbusho na
kuweza kushiriki mgomo huo
Daladala zikiwa zimepaki na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea Mwenge.
Daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho zimepaki baada ya mgomo wao wa leo mchana.
Daladala zikiwa zimepaki na kugomakupeleka abiria mwenge
Madereva na Makondakta wakizuia magari mengine kupita na kupeleka abiria
Waandishi wa Habari wakichukua Maelezo kutoka kwa kamanda wa polisi Kinondoni kuhusu mgomo huo wa daladala uliofanywa leo mchana na madereva wa magari ya Tandika,Mbagala,Buguruni ambayo yanatumia kituo cha Makumbusho kushusha abiria
Madereva wa daladala kwa mbaliiii kama wanavyoonekana wakiendelea kuongea na Viongozi wa Serikali kuhusu Tatizo lao la barabara mbovu ya makumbusho kuelekea mwenge
Madereva na Makondakta wa mabasi yanayofanya Safari zake kati ya mbagala,tandika kupitia kituo cha makumbusho wakijadiliana na viongozi wa sumatra na polisi Ili kuweza kujua watatoa Suluhisho gani ili kuweza kutatua tatizo la barabara mbovu eneo la makumbusho
Madereva na Makondakta wa mabasi yanayofanya Safari zake kati ya
mbagala,tandika kupitia kituo cha makumbusho wakijadiliana na viongozi
wa sumatra na polisi Ili kuweza kujua watatoa Suluhisho gani ili kuweza kutatua tatizo la barabara mbovu eneo la makumbusho
Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta
Kamanda wa Polisi kinondoni akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari baada ya kuweza kukubaliana na Madereva na Makondakta kutumia barabara kuu kwa siku mbili ili wakati wakiendelea kushughulikia utaratibu wa kutengenezwa kwa barabara za ndani ambazo walikuwa wanapaswa kuzitumia
PICHA NA HABARI NA DJ SEK BLOG
No comments:
Post a Comment