Kundi la watalii wa ndani ambao minongoni mwao walikuwa ni Askari kutoka chuo cha taaluma ya Polisi Moshi wakipanda kuelekea Shira Hut moja ya kilele katika Mlima Kilimanjaro.
|
Ofa ya utalii wa ndani katika mlima Kilimanjaro ilijumuisha watu wa Kila Rika,hapa mmoja wa watalii wa ndani akiwa na mtoto wake mgongoni.
|
Kiasi safari ilikuwa ngumu kwa baadhi ya watalii wa ndani
|
Kila hatua zilizo pigwa wataalii wa ndani walipenda kuchuku Taswiras.
|
Na safari iliendelea hapa ikiongozwa na mkufunzi mkuu wa chuo cha polisi Moshi ,SSP,Grayfton Mushi.
|
Baadhi ya watalii walionekana kuchoka lakini kila walipoulizwa walidai wameweka pozi la picha.
|
Safari ya baba na mwana iliendelea ,Mgongoni ni Mtoto Matinde Chacha akiwa na baba yake John Chacha.
|
Hatimaye watalii wakafika Shira Hut,wengine wakiwa wametupia mavazi ya Suti.
|
Afande akiwa hoi baada ya safari ya saa moja ya kufika Shira Hut.
|
Waliofika wakafurahia madhari nzuri na kupata Taswira ya pamoja.
|
Safari ya kuelekea katika mapango ya Shira(Shira Caves)ikaanza tena kutoka Shira hut.
|
Mkuu wa mafunzo katika chuo cha taaluma ya Polisi ,Grayfton Mushi akipozi huku mwenzake Moses Ruvinga ambaye pia ni afisa katika chuo hicho akichukua taswira.
|
Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa ndani ya moja ya Mapango ya Shira yaliyoko katika mlima Kilimanjaro.
|
Watalii wa ndani wakiwa katika eneo hilo la Mapango.
|
Watalii wa ndani wakatembelea eneo la Shira Camp kujionea watalii wanavyo lala wakati wakifanya safari ya kuelekea katika kilele cha Kibo .
|
Hapo wakakutana na Wabebaji wa mizigo ya watalii maarufu kama Wagumu na kupata nyinmbo mbalimbali.
|
Waliopanda na vazi la Suti wakaonesha vipaji vyao vya kusakata Kiduku,
|
Wengine walipata fursa ya kupiga picha na watalii waliokuwepo katika kituo hicho.
|
Kutokana na kuchoka wengine waliamua kupumzika katika machela maalum ya kushushia watu waliozidiwa mlimani.
|
Baadae safari ya kurudi toka mlimani ikaanza.
|
No comments:
Post a Comment