HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 28, 2014

WATANZANIA WAISHIO LONDON WAFANYA SALA MAALUM YA KUILIOMBEA TAIFA

Na Freddy Macha

Alhamisi jioni, Wazalendo na marafiki zao walishiriki misa kuiombea Tanzania ndani ya kanisa mashuhuri la Westminster Abbey kuadhimisha miaka 50 ya muuungano. Westminster Abbey-pic by F Macha 2014  
Misa hizi hutayarishwa kila mwaka kwa heshima ya nchi za Jumuiya ya Madola. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Peter Kallaghe( pichani chini akisalimiana na baadhi ya walioshiriki), maofisa ubalozini na wawakilishi wa Jumuiya ya Uingereza na Tanzania (British-Tanzania Society). Balozi Kallaghe na Watanzania Wahindi Westminster- pic by Rashid Dilunga 2014 Kwaya ya Chuo cha Lancing, iliimba nyimbo za kizamani za Kizungu na Kikristo katika mahadhi yaliyorembwa na vinanda na maandiko matakatifu. Westminster Abbey iliyo eneo la majengo mahsusi ya kiserikali na saa maarufu - Big Ben, iliasisiwa mwaka 1245 na Mfalme Henry wa Tatu. Misa-2-pic by F Macha  
Ni moja ya majumba yanayothaminiwa na kuheshimiwa sana tena sana Uingereza. Toka mwaka 1066 watawala wa kifalme, watu mashuhuri na muhimu nchini huzikwa ndani humo.Balozi Kallaghe na BTS - Trevor Francis katikati-pic by R Dilunga 2014 Balozi Kalaghe akitoka kanisani na wananchi. Katikati ni Trevor Francis wa British -Tanzania Society (BTS). Picha na Rashid Dilunga
Kati ya waliozikwa hapa ni William Shakespeare na Charles Dickens (waandishi mashuhuri) ;mmisionari aliyesafiri Afrika Mashariki na Kati karne 19, Dk. David Livingstone; wanasayansi Isaac Newton na Charles Darwin. Vile vile Waziri Mkuu Wiston Churchill aliyeongoza taifa hili wakati wa vita vikuu vya pili vya Wazungu (1939-45). Mwili wa Baba wa taifa Mwalimu Nyerere uliwekwa hapa kutazamwa na kadamnasi kabla ya kusafirishwa Tanzania, Oktoba 1999. Westminster Abbey- by F Macha 2014 Sala maalum kwa ajili ya marehemu Nelson Mandela ilifanywa Westminster mwezi Machi mwaka huu. Mbali na misa na mazishi -Westminster Abbey huwa ukumbi wa sherehe maalum. Mathalan miaka ya karibuni ndoa za mtoto wa Malkia Elisabeth (Prince Charles na Diana, 1981) na mjukuu William (2011) na Catherine, zilisheherekewa hapa. Akizungumza kwa Kiswahili na Kiingereza baada ya sala, Balozi Kallaghe aliwashukuru wote waliohudhuria. “Ni heshima iliyoonyeshwa na watu wa madhehebu mbalimbali kujumuika pamoja kuombea taifa letu na kumtakia kila Mtanzania mazuri,” alisema. Watanzania waliohudhuria wakitoka W Abbey- pic by R Dilunga 2014 Kati ya Watanzania niliozungumza nao ni Zarina na Zehra Jafferji wa dhehebu la Kibohra waliolitakia taifa letu mema na mfanyabiashara Abubakari Faraji na Mariam Kilumanga wa jumuiya ya wanawake London (TAWA). “Watanzania ni ndugu moja,” alisema Mariam Kilumanga. “Ndani ya familia yangu tunao watu wa dini kadhaa bila ubaguzi.” Misa-1Mtanzania mshindi wa taji la Jumuiya ya Madola la Africa (Miss Commonwealth Africa 2013) Malkia Kassu, alisema ni kitendo cha amani kuwa ndani ya Westminster Abbey na ishara ya matumaini kwetu sote.Balozi na Watz- Westminster-pivc by R Dilunga Picha ya pamoja ya baadhi ya wahudhuriaji. Imepigwa na Rashid Dilunga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad