Baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Shanghai nchini China wamesherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania kwa kukutana pamoja na kuzungumza mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Licha ya sherehe hizo za Miaka 50 ya Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kumaliza mwaka huu.
Baadhi ya Watanzania waishio Shanghai wakipiga picha ya pamoja katika shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanzania,yaliyofanyika jana.
Baadhi ya Watanzania wanaomaliza masomo yao mwaka huu wakipiga picha ya pamoja mbele ya keki ya Muungano.
Mmoja wa wahitimu Bi. Hellen Shayo akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Watanazania waishio Shanghai cha kuwa mwanachama hai kwa kipindi chote alichokuwa hapa.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria sherehe za Muungano.
Watanzania wakikata keki ya Muungano huku wakiwa wa nyuso za bashasha zinazodhihirisha umuhimu wa siku hiyo adhimu.
Wakipata chakula.
wakiyarudi magoma kusherehekea Muungano.
Mdau wako wa nguvu akifurahia siku hii adhimu.
Baadhi wageni waalikwa.
Guys, we are proud of you.
ReplyDeletehivi ndivyo inatakiwa. sio malumbano kibao. tuige mfano huu Tz yetu itafika mbali. Asante vijana
ReplyDeleteHongera san Uongozi na Watanzania huko mnaouenzi Muungano.
ReplyDeletewe are proud of you guyz. serikali ikumbuke watu kama hawa wanaoitangaza vyema nchi yetu