Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akihutubia wananchi wa Manispaa hiyo (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Afya Bonanza linalofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kupima afya bure wananchi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akitoa maelezo ya utangulizi kwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Bonanza hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizindua rasmi zoezi la upimaji afya.
Bi. Sophia Mjema naye akipima kipimo cha shinikizo la damu.
Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya vipimo.
Wananchi wakisubiri kuitwa kwa namba kwenda kupata ushauri wa kitaalam wa kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya hiyo.
Wananchi wakiwa katika huduma.
No comments:
Post a Comment