Huu ni Uchafu ukiwa nyuma ya kituo cha Daladala cha Biafra,Kinondoni jijini Dar es Salaam kama ulivyonaswa na kamera mani wetu na ukitizama picha vizuri kuna abiria amekaa lakini cha kusikitisha nyuma yake kuna uchafu ambao unatoa harufu mbaya na pia kuna wafanya biashara katika eneo hili. Sehemu hii imekuwa kero kwa abiria wanaoshuka na hata wanaopanda magari kwenye hiki kituo cha Biafra kwani kuna uchafu mwingi unaotupwa na wakazi wa maeneo ya jirani na kituo hicho,hali iliyopelekea kituo hiki kubadilishwa na kuonekana kama dampo.
Hii ndio hali halisi ya kituo cha Daladala cha Biafra kilichopo kwenye wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kilichogeuzwa kama sehemu ya kutupia takataka.
Jambo la kujiuliza ina maana hapa Biafra hakuna Dampo? Au uongozi wa eneo hili umelala mpaka kituo hiki kuwa na hali kama hii inasikitisha sana.PICHA NA PAMOJA BLOG




No comments:
Post a Comment