HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 16, 2013

MPANGO WA “Matokeo makubwa Sasa”“Big Result now”KATIKA SEKTA YA ELIMU WAZINDULIWA JIJINI DAR

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawabwa akifafanua jambo wakati akizindua wa utekelezaji wa mikakati ya “Matokeo makubwa Sasa” ambapo kwa kingeleza unaitwa “Big Result now” katika sekta ya elimu. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi mpya wa mwalimu Nyerere,jijini Dares salaam jana. mpango huu utaongeza fursa za ukuaji uchumi wananchi na kuchochoea ustawi kwa maisha bora kwa watanzania wote. 
Baadhi maafsa wa Elimu mikoa wakisaini nakala za ahadi za mpango huo(wakwanza kulia)Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Bw,Hirson Kipenya ,akifuatiwa na,Yusufu Kipengele, Mkoa wa Pwani ,Ibrahim Mbango,Mkoa wa Manyara,wanaoshuhudi (wakwanza kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawabwa(katikati) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo(wakwanza kushoto)Naibu waziri wa Tamisemi Mhe, Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa
Maafsa wa Elimu mikoa wakitoa ahadi zao kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dk Shukuru Kawabwa namna watakavyoenda kutekeleza mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa”katika sehemu zao za kazi.
Wadau wa Elimu wakiwa kwenye mkutano huo wakati wa uzinduzi wa “Matokeo makubwa Sasa” ambapo kwa kingeleza unaitwa “Big Result now”kwa sekta ya Elimu.
kikundi cha ngoma Parapanda kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad