Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira na Usalama, Bi. Tumpe Mwaijande akiongea na wafanyakazi wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara (hawapo pichani) hiyo baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Buguruni Bahresa leo asubuhi. Pamoja na zoezi la Usafi Wizara ya Uchukuzi ilikabidhi Majembe, mafyekeo na reki kwa Shule ya Msingi Hekima na Zahanati ya Buguruni.
Wafanyakazi
wa Wizara ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa ndani ya
Treni kuelekea katika kituo cha Buguruni Bahresa, ambapo waliadhimisha
Wiki ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi katika eneo hilo leo
asubuhi. Kauli Mbiu ya Wizara katika siku hii ni "Hifadhi maazingira kwa
Uchukuzi Endelevu". Aidha Kauli mbiu ya Kitaifa ni 'Fikiri, kula;
hifadhi Mazingira".
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman Kisamfu (wa
pili kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (wa tano kutoka kushoto) wakisubiria
kuanza kazi ya Usafi katika eneo la Stehseni ya Buguruni Bahresa. Wizara
ya Uchukuzi na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wamefanya usafi
kwenye eneo hilo leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya
Mazingira Duniani mbayo kitaifa inaadhimishwa Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira na Usalama wa Usafiri Majini, Bi. Tumpe Mwaijande
(aliyeshika mfuko) akifanya usafi katika eneo la Buguruni Bahresa kama
ishara ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani. Wafanyakazi wa wizara
ya Uchukuzi pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo walifanya
usafi katika eneo hilo kama ishara ya kuadhimisha siku ya Mazingira
Duniani ambapo Kauli mbiu ya Wizara hiyo ikiwa ni "Hifadhi Maazingira
kwa Uchukuzi Endelevu".
Wafanyakazi
wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifanya
usafi katika Stesheni ya Buguruni Bahresa kama ishara ya kuadhimisha
wiki ya Mazingira Duniani, Zoezi hilo la kufanya usafi limebeba kauli
mbiu inayosema "Hifadhi Maazingira kwa Uchukuzi Endelevu".
No comments:
Post a Comment