HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 14, 2013

WATOTO WATAKA MILA POTOFU ZIONDOLEWE

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Watoto wa mkoa wa Dar es Salaam wametoa ombi kwa Serikali Pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuondoa mila potofu ambazo zimekuwa zikileta madhara kwa watoto mbalimbali hapa nchini pamoja na kusimamia sheria zinazowalinda watoto.

Watoto hao wameyasema hayo wakati wa Kongamano la watoto Mkoa wa Dar es Salaam lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Plan kwa kushirikiana na mashirika mengine kwa lengo la kuwajengea watoto uelewa wa haki zao na wajibu wao katika maisha yao ya kila siku.

Watoto hao ambao wametoka katika Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke kwa kushirikisha makundi mbalimbali na walezi waliweza kutumia fursa hiyo kuiomba serikali na halmashauri kutunga sheria ndogondogo ili wale wote watakaovunja haki za watoto waweze kuchukuliwa hatua.

Aidha wameomba kufanyika midahalo ya mara kwa mara itakayowakutanisha watoto na kuwasikiliza shida zao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha ya kila siku na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.

Vilevile baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam ambao walikuwa wakishiriki katika kongamano hilo walionyesha kufurahishwa na mkusanyiko huo ambao uliwawezesha kutoa maoni yao na kusikilizwa na mashirika yaliyoshiriki kongamano hilo.
Baadhi ya watoto walioshiriki Kongamano la watoto mkoa wa Dar es Salaam lililoandaliwa na Shirika la Plan kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kutambua haki zao na wajibu wao.
Baadhi ya wadau wa watoto walioshiriki Kongamano la watoto mkoa wa Dar es Salaam lililoandaliwa na Shirika la Plan kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kutambua haki zao na wajibu wao.
Baadhi ya watoto walioshiriki Kongamano la watoto mkoa wa Dar es Salaam wakiimba wimbo wakati wa kongamano hilo, kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la Plan kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kutambua haki zao na wajibu wao.
Mtoto mmoja wapo aliyeshiriki Kongamano la watoto mkoa wa Dar es Salaam akijielezea mbele ya watoto wengine wakati wa kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Plan kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto kutambua haki zao na wajibu wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad