Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Coast,Traore Lacina akiwania Mpira wa juu na Beki wa Timu ya Taifa,Shomari Kapombe wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2014 kule nchini Brazil uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mpaka mwisho wa Mchezo,Taifa Stars ililala kwa Mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast.
Mshambuliaji Thomas Ulimwengu akiondoka na Mpira huku Beki wa Ivory Coast akitaka kumkwatua kwa nyuma bila Mafanikio.
Mtanange ulikuwa ni mzuri na wakuvutia,kani timu zote zilikuwa zikicheza kwa kasi sana.
Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Coast,Yao Gerveis akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Taifa Stars,Frank Domayo wakati wa Mchezo huo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Chenga za hatari mpaka mtu anakaa chini.
Beki sifa kwake hata sio lazima,hapa ni Beki wa Timu ya Ivory Coast akijaribu kuondosha hatari langoni kwake.
Kiungo wa Kimataifa kutoa Ivory Coast,Yaya Toure akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Taifa Stars,Frank Domayo wakati wa Mchezo huo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Imepigwaaaa moojaaaaa paleeeeee Gooooooooo...... Daaahhhh,inakenda nje.
Nani alisema urefu ni Dili??sasa Muone Aboubakar Salum a.k.a Sure Boy akiwachachafya mabeki wa Ivory Coast.japo wametufunga Bao 4-2 lakini chenga zetu za maudhi wamezipata.
Beki hasifiwiiiii.....
Jamaa ilifika kipindiwakaanza kutia Kabali,maana gemu kwao lilishaanza kuwa gumu.
Wamejipangwa kwa kuzuia shuti.
Wazee wa Kazi mzigoni.
Bendera yetu ikikatiza walikokaa wao.
Msema mungu mpenzi wa kweli,Pamoja na Kufungwa lakini shangwe zilikuwa ni Mwanzo mzishooo....
Kipa wa Ivory Coast akidaka mkwaju mmoja uliopigwa na Mshambuliaji,Thomas Ulimwengu.
No comments:
Post a Comment