HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 15, 2013

Show ya Lady Jay dee ni hatari tupu ndani ya Nyumbani Lounge usiku huu

 Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
 Getini mambo yako namna hii.
 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

Kwa picha na video zaidi zitawajia baadae kidogo.

2 comments:

  1. Wanafiki wa "Kelele FM" na Mwana NAFAKA Wao wanune tu

    ReplyDelete
  2. Hayaa nashkuru kwa taarifa , lakini huku ni kutokujiamini kwa nini asingekodi ukumbi unaoeleweka ....

    ReplyDelete

Post Bottom Ad