Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mh. Mwantumu Mahiza akihutubia katika mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya uliofunguliwa leo mjini Kibaha,mkoani Pwani.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Mohammed Hashim (kulia) akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza baada ya kufungua mkutano wa wadau wa mkoa huo wa kujadili uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko huo, leo mjini Kibaha. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akielezea mikakati mbalimbali ya kuboresha mfuko huo nchini,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya uliofunguliwa leo mjini Kibaha,mkoani Pwani.
Mbunge wa Kibiti, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Pwani, Abdul Marombwa akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa hotuba yake pamoja na ujio wa NHIF mkoani humo.
Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani,Andrew Mwilungu akiwakaribisha wadau kwenye mkutano huo muhimu wa uboreshaji wa sekta ya afya kwa wananchi kujiunga NHIF,CHF pamoja na TIKA mkoani.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Ofisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Kisinga (kulia)
akiratibu mkutano huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Hamis Mdee na Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani, Andrew Mwilungu.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Ahmed Kipozi na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu.
Viongozi wa NHIF, CHF wakiwa pamoja na wadau kwenye mkutano huo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
No comments:
Post a Comment