HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 10, 2013

Mgodi wa Geita wajiandaa na Kilimanjaro Challenge 2013

 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani akiwatambulisha watoto yatima Irene Joachim Katikati na Geofrey Yohana watakaopanda mlima Kilimanjaro katika kuhamasisha taasisi na mashirika mbalimbali kuchangia fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi nchini Tanzania hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine.
 Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma Mrisho (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar Issa wakimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 15,000,000 Sister Adalbera Mukure wa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Moyo wa Huruma cha Geita wakati wa hafla maalum ya kukabidhi fedha hizo kwa mashirika mablimbali yanayopambana na ugonjwa wa ukimwi iliyofanyika Ijumaa kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam fedha hizo zinakusanywa Mgodi wa Dhahabu ya Geita Gold Mine na washirika wake kwa kupanda mlima Kilimanjaro
Kutoka kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar Issa, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma Mrisho,  wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa TACAIDS kutoka kulia ni Jumanne Issango  Mkurugenzi wa Uraghibishi, Beng’i Issa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na Moriss Lekule Mkurugenzi wa Mwitikio wa Taifa hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine.

Mgodi wa Geita umejiandaa na mwaka mwingine wa Kilimanjaro Challenge katika Hotel ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Tanzania Ijumaa iliyopita. Pia ufunguzi wa hafla huo ulihusisha kutaja majina ya asasi zitakazo faidika na fedha zilizokusanywa katika upandaji mlima mnamo mwaka wa 2012. 

 Mpango huu kwa mara ya kwanza ulianzishwa mnamo mwaka 2002 ukihusisha wapandaji mlima 47 uliowezesha kukusanya kiasi cha fedha za kitanzania milioni 62. Ni mafanikio hayo yaliyoipa nguvu na moyo Geita Gold Mine kufanya tukio hilo la upandaji mlima kama tukio la kitaifa la kila mwaka. Tangu wakati huo wastani wa wapandaji 50 mpaka 55 walijiunga na msafara huo kila mwaka. Hadi sasa, zaidi ya watu 500 kutoka duniani kote wameshiriiki katika kukusanya zaidi ya fedha za Kitanzania Billioni 2 ambazo zimenufaisha zaidi ya asasi zisizo za kiserikali 30 NGO nchi nzima katika kupambana na VVU/UKIMWI Tanzania. 

 “Lengo la Kilimanjaro Challenge ni kujenga uelewa zaidi juu ya janga la VVU/UKIMWI, kutoa msaada wa kifedha kwenye mpango huo na kujenga timu bora ya kitaifa katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.” Alisema Bwn. Godvictor Lyimo.

Mpango huu wa kujitolea na ule wa serikali unawapa nafasi wapandaji wa ndani kupanda mlima Kimlimanjaro. Katika miaka 11 iliyopita watu wengi wameshiriki katika kupanda mlima kwa kujitolea,akiwemo mvulana wa miaka 11 na mzee wa miaka 84, Raisi wetu Mstaafu Mhe. Mzee Ali Hassan Mwinyi. 

Kwa mujibu wa Waziri mkuu Mhe. Mizengo K. Pinda, uamuzi uliofanywa na Mzee Mwinyi ulikuwa ni wa kujidhatiti, akinukuu kauli ya ‘Mbiu ya Mgambo’ katika uamuzi huo. Kwa mujibu wa Bwn Godvictor Lyimo Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani GGM, “Imeripotiwa kwamba kiwango cha maambukizi kimepungua kutoka asilimia 13 mwaka 2000 hadi asilimia 7.8 mwaka 2007 na kwenda chini zaidi mpaka asilimia 5.1 mwaka huu 2013. 

Kama moja ya jitihada za kuongeza uelewa juu ya VVU/UKIMWI, Raisi Jakaya Kikwete alizindua kampeni ya upimaji wa hiyari wa VVU/UKIMWI kwa kutumia mwamvuli wa “Kilimanjaro Challenge” GGM mpango huu umepata mafanikio katika kutoa uelewa juu ya janga hili na tunaangazia kuendeleza jitihada hizi mpaka pale Tanzania itakapo tangaza kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ni sifuri.” 

Migodi ya Geita ipo kilometa nne Magharibi mwa Geita na Kasikazini Magharibi mwa Tanzania. Mgodi unamilikwa na AngloGold Ashanti Limited kwa asilimia 100. AngloGold Ashanti Limited ni kampuni ya kimataifa inayojivunia Afrika. Tunashughuli 20 ndani ya nchi kumi katika mabara manne , ikiwemo ufunguzi wa miradi. AngloGold Ashanti ni moja ya makampuni makubwa ya migodi ya madini ya dhahabu. Kwa habari zaidi tembelea: www.anglogoldashanti.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad