Katika heka heka na mishe mishe za mjini na kuhakikisha Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog linasonga,niliibuka sehemu na kukutana na hii stori nami nikaona sina sababu ya kuifaidi mwenyewe,ndio nimewaletea ili nanyi mjionee mambo ya kitaani.
Muvi lilianzia kwenye Daladala lililokuwa linatoka KARIAKOO - UBUNGO na anaeanza na sini ya kwanza ni Kondakta wa daladala hilo alaianza namna yake ya kuuliza vituo vya kushuka abiria,hii ni baada ya kufika MANZESE konda akauliza kuna mtu anashuka?
Dada mmoja kimbelembele akajibu tumeziacha nyumbani tuna mitandio tu hapa tulipo,yule konda alimcheki kwa jicho la tamaa sana lakini akaona sio ishu nae anauchuna tu.
Sasa kufika mbele kidogo tu,yule dada alie leta nyodo akawa ashasahu na hapo anashuka UBUNGO MAZIWA,akaanza kujinyanua kwenye kiti na kusema wee konda nashuka maziwa hapo.
Na hili ndilo jibu la konda wakati huo,akasema kayanunulie Sidiria yasishuke halafu huku akimwambia dereva kanyaga twendeeeee.........
Na hii ndio faida na hasara za nyodo na jeuri.
No comments:
Post a Comment