Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo(MB) Akiendesha kikao cha wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Baadhi ya Wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi,wakifatilia kikao hicho.
Na Abdulaziz Video,Ruangwa
Jumla
ya wanafunzi 212 Kati ya 449 wanaosoma kati ya darasa la tatu hadi la
saba katika Shule za Msingi za Nandagala na Mkata Wilayani Ruangwa,
Mkoani Lindi hawajui kusoma wala kuandika huku wengine 15 ambao
wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu huku wakiwa
hawajui kusoma wala kuandika.
Hayo
yamebainika katika kikao cha wadau wa Elimu Wilayani Ruangwa kilichokaa
chini ya Mwenyekiti wake,Mkuu wa Wilaya hiyo Agness Hokororo Kupokea
taarifa za hali ya Elimu na kutafuta Ufumbuzi wa chaongamoto
zinakwamisha Elimu Wilayani humo kilichofanyika jana.
Wakichangia
katika kikao hicho Baadhi ya Wadau wakiwemo Madiwani wa Halmshauri hiyo
walieleza kuwa Mwamko Mdogo wa Wazazi na Uwezo mdogo wa Walimu katika
Ufundishaji ikichangiwa na Upungufu mkubwa wa walimu pamoja na Mila na
Desturi ni baadhi ya changamoto zinazokwamisha ukuaji wa Elimu Wilayani
Humo.
Andrew
Chikongwe,Diwani Kata ya Nandagala alisema kuwa tatizo lipo kwa walimu
kwani wengi wao hawajitumi katika ufundishaji licha ya kuwepo kazini
muda wote hali inayoonyesha kuwa wana mgomo baridi. “Pamoja walimu
kuwepo kazini lipo tatizo la kutojituma katika ufundishaji hii
inachangia sana watoto wetu wafanye vibaya”alisema Chikongweali.
Naye
Juma Nampupanga ambaye ni Mfanyabiasharaalisema kuwa kutotilia mkazo wa
elimu miongoni mwa wananchi ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya watoto
wetu kwani wananchi wengi wa wilaya ya Ruangwa hawana mwamko wa elimu
kwani si kipaumbele cha hivyo kutofuatilia maendeleo ya watoto.
Ibrahimu
Ndoro Diwani wa Kata ya Ruangwa aliitaka serikali kuwachulia hatua
baadhi ya walimu wanaopangwa kufanya kazi katika Wilaya za mikoa ya
kusini ambao mara wakisharipoti huwa wanaondolka kwa kisingizio cha
kufuata familia zao na badala yake hawarudi tena na kufanya wilaya hizo
kuendelea kuwa na upungufu wa waalimu.
Akizungumza
kwenye mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Agnes Hokororo aliwataka
wananchi na viongozi kushirikiana katika kuondoa changamoto mbalimbali
zinzosababisha maendeleo mabaya ya elimu wilayani humo.
“Iwapo
viongozi tutashirikiana maendeleo ya elimu wilwywni kwetu yatakuwa
mazuri kwani suala la maendeleo ya elimu ni la kila mmoja wetu”alisema
Hokororo
No comments:
Post a Comment