Menejimenti
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutaarifu umma wa Watanzania
kuwa tangazo la nafasi za ajira ambalo limewekwa katika mtandao www.eastafricajobscarieer.com ni batili.
Mtandao huo ulichapisha tangazo hilo bila ridhaa ya Menejimenti ya Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hauna mkataba wowote wa
kibiashara na mtandao huo.
Aidha,
tangazo hilo ni nakala ya tangazo la ajira ambalo Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya ulilitangaza katika magazeti ya Mwananchi, Nipashe, na Daily News tarehe
07, 10 na 14 Februari, 2012 na mchakato wa kujaza nafasi zilizotangazwa
ulishakamilika.
Menejimenti
ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya inawaomba radhi wote ambao wamepata usumbufu
kutokana na tangazo hilo.
Limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
S.L.P. 11360,
DAR
ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment