HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 4, 2013

MVUA YAWALIZA WANANCHI WA KYELA MKOANI MBEYA

Na Edwin Moshi, Kyela 

WANANCHI  wa Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani Mbeya wapo hatarini kukumbwa na baa la njaa sambamba na kukosa mahala pa kuishi kutokana na mazao yao pamoja na nyumba zao za kudumu kusombwa na mvua za mafuriko yaliyotokea  siku tatu mfululizo na kuleta maafa makubwa kwa wakazi wa Tarafa hiyo,

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Makwale Tarafa ya Ntebela Evance Mwaipopo wakati akizungumza na mtandao huu ulipotembelea katika Tarafa hiyo mara baada ya kutokea mafuriko hayo,ambapo alidai kuwa mvua hizo za mafuliko zimeleta maafa makubwa kwa wakazi wa Kata hiyo na Tarafa kwa ujumla,

Alisema kuwa mvua hizo zilizoleta mafuliko yaliyosababisha baadahi ya mito ukiwema mto Lufilyo kuhama katika njia zake za asili na kupasua kuelekea katika makazi ya watu na kusababisha maafa makubwa ya kuharibu nyumba zaidi ya 200,na mazoa ya chakula ya muda mfupi kama mpunga,mihogo na viazi,na mazao ya muda mrefu kama michikichi,miembe na miti mingine ya matunda,ambayo yote imesombwa na maji,

Awali aliongeza kuwa kulitokea na mafuliko kama hayo yaliyoleta maafa ambapo yaliharibu mazao kama hayo pamoja na makaburi 30 na jengo la Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na ofisi ya Kijiji cha Ngeleka one,ambavyo vyote vilisombwa na maji kufuatia mafuliko hayo,

‘’Ni kweli  wananchi wa tarafa hii wapo katika hatari ya kukubwa na baa la njaa kufuatia kukumbwa na maafa haya na wengine wakikosa makazi ya kudumu kutokana na nyumba zao kusombwa na maji,lakini taarifa za maafa haya tumezipeleka serikalini ili kujua namna watakavyo weza kuwasaidia waathirika hao’’alisema Mwaipopo,

Diwani  wa kata ya Makwale Alico Kasyupa kwa upande wake alisema kuwa mafuliko hayo yalianza kwenye kata yake ambapo aliwaamuru wakaza wa kata hiyo waliojenga pembezoni mwa mto huo kuyahama makazi hayo ambapo tayali zoezi hilo limefanyika huku wengine walilazimika kubomoa nyumba zao na kuzijenga katika maeneo ya mwinuko ili wasikumbwe na mafuliko hayo,

Alisema kuwa hivi sasa mvua hizo za mafuriko zimeendelea kuleta maafa makubwa katika kata zingine hususani Tarafa nzima ya Ntebela huku idadi ya waathirika ikiongezeka kutokana na nyumba zao kubomoka ikiwa ni pamoja na mazao ya chakula yaliyokuwa tayari yameanza kukomaa,huku huduma za usafiri kutoka Ipinda Matema zikisimama,

Aliongeza kuwa Serikali Wilayani Kyela imepata taarifa ya uwepo wa maafa hayo na inafanya juhudi za kujua namna ya kukabiliana na maafa hayo ikiwa ni pamoja na kuurudisha mto huo katika njia yake ya asili ili usiendelee kuleta maafa zaidi,

Wananchi wa Tarafa hiyo kwa upande wao wameilalamikia Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuwa wazito kulitafutia ufumbuzi suala hilo,huku wakiendelea kuteseka bila msaada kutoka katika Serikalini,na kwamba wameitaka Serikali wilayani hapa kuliangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo ili kujua ni namna gani watawasaida wananchi waliokumbwa na maafa hayo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad