HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 12, 2013

Mtanange wa Taswa na Bongo Movie ulivyokuwa

Wachezaji wa timu za Taswa FC (wenye jezi za bluu) pamoja na wapinzani wao wa Bongo Movie,wakisikiliza kwa makini maelekezo toka kwa refarii wa mchezo huo ambaye alikuwa ni Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Ally Kiba (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa mtanange wao ulipigwa kwenye Viwanja vya Sigara (TCC),Chang'ombe jijini Dar es Salaam jana jioni.Mtanange ulikuwa ni mkali sana kwa pande zote mbili na hadi mwisho wa mchezo timu ya Bongo Movie iliibuka kidedea kwa bao 2 - 0.hii ikiwa ni kwa upande wa mpira wa miguu lakini katika mpira wa pete,timu ya Taswa Queens iliibanjua timu ya Bongo Movie kwa Mabao 38 - 10.
Mtanange ulianza kwa kasi kubwa na ya ajabu kama ionekanavyo hapa.
Straika wa timu ya Taswa FC,Juma Pinto akichuana vikali na Beki wa timu ya Bongo Movie (ambaye hajawahi kuonekana kwenye movie) wakati wa mtanange wao uliopigwa jana jioni kwenye Viwanja vya Sigara (TCC),Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Watazamaji upande wa Taswa FC.
Watazamaji upange wa Bongo Movie.
hapa ni bambi kwa bambi,huku Refa akiangalia kwa makini kuona kwamba hachezewi mtu faulo.
Taswa FC kwa chenga tu hawajambo.
Aaaahhh...... Refaaaaa mbona ile penati sio halali???? Refa hana habari na mtu.
Ankal akisabahina na wadau.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad