HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 24, 2013

MRADI WA UENDELEZAJI MIJI TANZANIA (TSCP) WAENDELEA KWA KASI

Timu ya wataalamu kutoka OWM-TAMISEMI-katika Mradi wa Mpango Miji Mkakati (TSCP ) Pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia pamoja na Ubalozi wa Denmak wakikagua Ujenzi wa Barabara zinazoendelea kujengwa kupitia mradi wa TSCP katika Mnispaa ya Mtwara Mikindani katika kubaini utekelezaji na maendeleo ya maeneo mbalimbali ya mradi.
Wafanyakazi wa TSCP na Mwakilishi wa Benk ya Dunia wa kwanza kulia wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa maendeleo ya Mradi wa TSCP katka Mnispaa ya Mtwara Mikindani katika kubaini utekelezaji na maendeleo ya maeneo mbalimbali ya mradi.
Ujenzi wa kituo cha basi cha kigoma ujiji ukiendelea.


Toka uzinduzi wa mradi wa uendelezaji Miji. Tanzania Strategic Cities Project (TSCP), mnamo mwaka 2010. Mradi umekuwa ukiboresha huduma za msingi mijini kufikia walengwa. Mradi huu wa uendelezaji miji Tanzania umeundwa kwa ajili ya kukabili changamoto mbalimbali za Miji ya Tanzania. Mradi huu unatekelezwa na Halmashauri nchini, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi. 

Mradi huu ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na ruzuku kutoka Danida. Mwanzoni mwa wiki mwandishi wetu aliongea na Kaimu Katibu Mkuu wa Tamisemi Bwn. Jumanne Sagini ambaye alikua na haya ya kusema “Mradi wa uendelezaji miji Tanzania upo na una lengo la kuboresha viwango na kurahisisha ufikiwaji wa huduma za msingi Mijini kwa kukarabati na kupanua miundombinu ya Miji pamoja na kuziimarishia uwezo taasisi husika katika kuboresha mapato na usimamizi wake” Bwn. Jumanne Sagini aliendelea kusema “Mradi huu umegawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni Miundo mbinu na huduma za miji; 

Uimarishaji wa Taasisi pamoja na Usimamizi wa Mradi; na ni miji saba tu ndiyo itakayofaidika na mradi huu. Miji yenyewe ni Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Mtwara, na Dodoma, Kwa Mji wa Dodoma, Mradi unatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa Dodoma Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA)”. 

Mradi huu unagharama ya $ 175.5, ambapo $162.8 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na $12.7 ni ruzuku kutoka DANIDA. Mkopo wa Benki ya Dunia ni kwa ajili ya maeneo ya Miundombinu na huduma za miji, wakati ruzuku kutoka DANIDA itagharamia uimarishaji wa Taasisi katika kutekeleza majukumu yake. Ili kujua kwa undani zaidi kuhusu mradi huu, Mwandishi wetu wa habari aliongea na Mratibu wa mradi huu Mhandisi Davis Ben Shemangale. Mhandisi Davis Ben Shemangale alielezea 

 “Mradi huu ni njia ya kutekeleza dhana ya kugatua madaraka toka Serikali Kuu kwenda kwa umma, mradi huu wa TSCP unaendeshwa na Halmashauri husika kwa kuchagua na kuitekeleza miradi kwa kadri ya vipaumbele vyao”. 

Mhandisi Davis Ben Shemangale alimalizia kwa kusema “mradi huu umewekwa katika awamu tatu hadi nne kwa kila mji na mpaka sasa wakandarasi kwa awamu zote wamekwisha anza kazi” aliendelea kwa kusema “wakandarasi kwaajili ya kutekeleza awamu ya kwanza walianza kazi Novemba mwaka 2011 na awamu ya pili walianza kazi mwezi June mwaka 2012 ambapo awamu ya tatu na ya nne walianza kazi mwezi Novemba 2012”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad