HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 7, 2013

Taswira zilizonaswa na Kamera ya Mtaa kwa Mtaa leo

 Kama kawa kama dawa,leo katika pita pita zangu lilikatiza mtaa wa Samora avenyuu,uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam na kukutana na taswira hii ambayo niliona sina budi kuinasa na kuja kushea nanyi wadau hapa mtaani kwetu.hii gari ambayo namba zake za usajili zinaonyesha dhahiri kuwa ni mali ya Serikali,ilikuwa imepaki katika sehemu isiyoruhusiwa kama kibao kinavyoonyesha hapo na dereva wake kuendelea na shughuli zake kana kwamba kaegesha gari yake katika sehemu salama.baada ya muda kidogo wakakatiza wale Askari wa Jiji (Mgambo wa City) wakina na minyororo mikononi,walipoona gari hii imepaki hapo na mwenyewe hayupo,wakaipiga nyororo tairi na kuondoka zao kama alivyoondoka Dereva wa gari hiyo,huku wakiacha karatasi yao inayoelezea mahala husika pa kwenda kulipia faini ya kosa hilo katika kioo cha mbele cha gari hilo.
 Gari ikaendelea kukaa hapo huku ikiwa imepigwa nyororo kama ionyekanvyo pichani.
Baadae Dereva wa gari hilo akaja na kwa bahati nzuri yule Mgambo alieipiga pini alikuwa akikatiza eneo hilo,na kuanza kuzungumza ili kama vipi mambo yaishie juu kwa juu.sasa sijui nini kiliendelea baadae maana kamera man aliendelea na hamsini zake.
Lakini mbele ya gari lile kulikuwa na hizi ambazo hazikuguswa pamoja na kwamba zote zilikuwa katika mlolongo huo huo,sasa sijui jamaa walisahau au waliamua kuzichunia tu kwa kuwa walishaipiga pini moja wapo.ni hayo tu kwa leo wadau.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad