HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 29, 2013

Salaam za Lady Jaydee kwa wadau wa sanaa

Lady Jaydee

Katika mwaka huu wa 2013, inatimia miaka 13 tangu nianze  kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tuko pamoja na pia nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea kusupport muziki wa Tanzania na kunipa nguvu mimi kama msanii.

Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya muziki Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE katika muziki.

Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la 'NOTHING BUT THE TRUTH' ambayo ina jumla ya nyimbo 10.

Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.

Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu Awabariki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad