HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 23, 2013

Mzinga wa Boda Boda eneo la Kinondoni kanisani jioni ya leo

Jioni ya leo katika eneo la Kinondoni Kanisani kumetokea mzinga uliohusisha Basi aina ya Isuzu Journey lenye nambari za usajili T 721 APH na Pikipiki (bodaboda) yenye nambari za usajili T 717 CED na kupelekea Mwanadada mmoja (ambaye jina lake halikutambulika mara moja) aliekuwa amepakiwa kwenye Bodaboda hiyo kuvunjika mguu na kukimbizwa hospitali kwa matibabu huku dereva wa Bodaboda hiyo akionekana kuumia kidogo sehemu ya usoni.Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni Mwenyesha bodaboda huyo ambaye alionekana kuwa na haraka sana akitokea eneo la Kinondoni Morocco na kuvuka ghafra barabara kuu bila ya kuangalia magari yanayotokea Kinondoni Manyanya.hata hivyo,Dereva wa basi hilo alijitahidi kumkwepa bila ya mafanikio kutokana na kuwepo kwa mabari mengine upande wake wa kulia na ndipo akaivaa bodaboda hiyo iliyokuwa imepakia abiria huyo alievunjika mguu.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Mashuhuda wakiangalia tukio.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad