Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji wa vileo wakati walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) watengenezaji wa kileo cha Konyagi jijini, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Mahamoud Mgimwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda hicho jijini,Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited (TDL),jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakipita eneo la matanki ya uchachuaji wa bia walipotembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Makao Makuu ya kampuni hiyo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Phocas Lasway akitoa maelezo jinsi ongezeko la kodi ya asilimia 25 lililovyoathiri uzalishaji wa kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mgimwa akielezea jinsi watakavyoshirikiana na TBL kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazikabili kampuni hiyo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akizungumza wakati
wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara walipotembelea
kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), juzi katika Makao Makuu
kampuni hiyo, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo,
Ahmed Salum na Mahamoud Mgimwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Wanachama na Mawasiliano wa CTI, Neema Mhondo akielezea jinsi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilivyopandisha kiholela ada kwa kampuni mbalimbali kutoka sh. 400,000 hadi milioni 7 kwa mwaka.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

No comments:
Post a Comment