HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 1, 2012

WAZIRI MUKANGARA AWATAKA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA HABARI KUTEKELEZA VIPUMBELE MUHIMU

NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza vipaumbele muhimu vya wizara ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuwajengea maisha bora wananchi wake.

Akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa ili kufanikisha malengo na vipaumbele vilivyowekwa wizara yake inawategemea wafanyakazi hao ambao ni nguvu kazi muhimu katika kuleta mabadiliko ya utendaji kazi.

Amesema kuwa wizara pamoja na mambo mengine inatekeleza masuala mbalimbali yakiwemo uandaji wa mpango wa miaka 5 wa maendeleo ya michezo nchini, kuunda baraza la taifa la vijana, kupatia ufumbuzi tatizo la maslahi ya wasanii na kukamilisha mchakato wa kupata vazi la taifa.

“Ili kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele hivi kila mmoja wetu anawajibika kufanya kazi kwa bidii mahali pake pa kazi bila kutegea wala kusukumwa.” Amesema Mukangara.

Amesisitiza kuwa sekta ya michezo ikiimarishwa nchini vijana wengi watapata fursa ya kuendeleza vipaji vyao na hatimaye kupunguza tatizo la ajira jambo ambalo likifanyika katika tasnia ya sanaa vijana wengi wataweza kujiajiri na kujiongezea kipato.

Naye kaimu mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza kwa kwa niaba ya wajumbe wa baraza hilo amesema Baraza litatekeleza maagizo yaliyotolewa kwa vitendo ili kuleta maendeleo ya wizara na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad