HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 6, 2012

WAJASILIAMALI 11 WAKABIDHIWA RUZUKU ZA SAFARI WEZESHWA JIJINI MBEYA

Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Gabriel Mwalugaja Ubao wa kuchezea Darts wa kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Rose Maluila mashine ya kutengeneza Crips ya kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Vumilia Mtweve Viti,Meza,Krti za Bia na Jiko la Kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Bahati Mbata Cherehani za kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Phares Lyimo Compresor ya kutengenezea Ngoma za kisasa na mashine ya Welding baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa Mkoa wa Mbeya,Viongozi wa Tbl na Wajasiliamali mara baada ya makabidhiano ya ruzuku Mbeya mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi Wetu.

MEYA wa Manispaa ya Mbeya Mjini, Athanas Kapunga amewakabidhi wajasiliamali mbali mbali ruzuku za Safari Lager Wezeshwa kwenye Uwanja wa CCM Ilomba Mbeya Mjini mwishoni mwa wiki.

Wajasiliamali waliokabidhiwa ruzuku hizo ni Rose Eliudi alipata Mashine ya kutengeneza Crips, Benedict Matandiko alipata cherani za kisasa , Vumilia Mtweve alipata Jiko la kisasa,viti 100,mezazake na kreti mia za bia, Bahati Mbata alipata Cherehani za kisasa , Hellen Mwanguku alipata Jiko kubwa lakuwokea mikate, Felix Kamuhabwa alipata machine ya kukatia vyuma vya aluminiam na vifaa vyake, Festo Mwakasege alipata Camera Sony Pd 170, Phares Richard alipata mashine ya Welding na Compresa ya kupakia Rangi, Iradi Msemwa alipata mashine ya kuchania mbao,Compresa ya rangi na vifaa vyake , Gabriel Mwalugaja alipata viti 30 na meza zake na ubao wa kuchezea darts na Tatu Ngemela alipata cherehani za kisasa.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Meya wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga aliishukuru Kampuni Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager kwa kuwawezesha Wajasiliamali kusonga mbele kimaisha kuanzia familia zao,majirani pamoja na wafanyakazi watakaowaajili ambao watafaidika kupitia ruzuku hii na Taifa kwa ujumla kwani tutafaidika kupitia kodi.

Alisema Kapunga, Hongera TBL na Hongera Safari Lager na endeleeni kuwekeza katika kuwekeza Nchini Serikali iko tayari kuwaunga mkono mmasaa 24.

Wakazi wa Mbeya ambao mmewezesha kuweni mstari wa mbele kunywa Safari Lager kurudisha walichotoa na kuwahamasisha jamii ya Mbeya wanywe Safari Lager kwani matunda yake yanaonekanawazi alimaliza Meya Athanas.

Ofisa Biashara wa Jiji la Mbeya, Magreth Muzrai aliishukuru Safari Lager Wezeshwa kwa kumuinua Mkazi wa Mbeya, kuinua kipato cha wajasiliamali waliopata ruzuku wao familia zao na jamii zinazowazunguka na Mbea kwa ujumla.Pia aliwataka wakazi wa Mbeya kuitangaza Safari Lager kwani ni Mkombozi wa Maisha yao.

Mmoja wa Wajasiliamali waliopewa ruzuku hizo, Festo Mwakasege aliishukuru Safari Lager Wezeshwa na kuahidi kutumia vizuri ruzuku waliyopewa kwa manufaa yao wenyewe, majirani, jamii inayowazunguka na Watanzania kwa ujumla na kwa kuwahakikishia aliwataka Safari Lager wawatembelee ili kujua maendeleo yao.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukingo aliwashukuru wajasiliamali wote waliojitokeza kuujaza fomu,pia aliwashukuru walifaulu na kupata ruzuku na wali waliokosa wasichoke kujaza fomu tena kwani zoezi ni endelevu na mwisho aliwaomba wakazi wa Mbeya kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Safari Lager mahali popote watakapokuwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad