HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 11, 2012

Rais Kikwete na Makamu wa Rais waongoza shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Bob Makani leo jijini Dar

Rais Jakaya  Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe wakisaidiana na ndugu na jamaa wa Marehemu Bob Makani kushusha mwili wake tayari kwa shughuli ya heshima za mwisho leo mchana katika viwanja vy Karimjee jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu atasafirishwa kesho asubuhi kwenda Shinyanga kwa mazishi. Picha zaidi pamoja na video clips zinaandaliwa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililo na mwili wa Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),marehemu Bob Makani ambaye pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu,katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal,Mama Salma Kikwete,Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chadema leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambaye pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu,katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe kwenye.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi wa Chama hicho Bob Makani
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee leo.Picha na Freddy Maro,Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad