HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 6, 2012

Rais Kikwete aisaidia taasisi ya mkapa kuchangiwa shilingi bilioni 3.2 katika harambee

 Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Bw Deo Mwanyika, Makamu wa Rais wa  Kampuni ya Barrick Tanzania baada ya Kampuni hiyo kuchangia dola laki 5 za kimarekani na kuongoza katika harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa na Taasisi ya HIV/AIDS ya Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation) usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency. Kushoto ni Rais mstaafu, Benjamini Mkapa na kulia  Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Picha ya kuchora Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UNDI Consulting Group Limited, Injinia Philip Makoka baada ya kuinunua wakati wa Harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam kwenye Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency usiku wa kuamkia leo
 Rais Jakaya  Kikwete akimkabisdhi  moja ya vito Mkurugenzi Mtendaji wa Hotel ya Kibo Palace ya jijini Arusha Bw. Vincent Laswai baada ya kununua kwa Sh Milion 12 wakati wa harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa na Taasisi ya HIV/AIDS ya Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation)
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi jiwe la Tanzania aliyelinunua kwa dola za Kimarekani 13,000 wakati wa Harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam kwenye Hotel ya Kempinsik Dar es Salaam.Kulia ni Balozi Amy Mpungwe ambaye kampuni yake ya Tanzanite One ndio iliyochangia jiwe hilo
Rais mstaafu, Ali Hassani Mwinyi akimkabidhi Picha ya marais wanne Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited, Bw William Chiume baada ya kuinunua picha hiyo kwa Sh Milion 13 wakati wa Harambee ya kuchangia Fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa na  kwa Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS Foundation. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad