Na Mwandishi Wetu, Moshi
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewaomba Askari Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kusaidia kukomesha udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watoa huduma katika o wa madai yao.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Kanda ya Kilimanjaro Bw. Chritopher Mapunda wakati akitoa elimu ya Bima ya Afya kwa Maofisa wa Polisi katika Chuo cha CCP Moshi, na askari katika Wilaya za Hai na Siha.
“Kumeanza kujitokeza wimbi la baadhi ya watoa huduma kutokuwa wakweli wakati wa uwasilishaji wa madai yao, tunawaomba sana ndugu zetu askari na wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa ujumla kutupatia taarifa pale tunapohitaji au unapoona kuna utata wa huduma,” anasema Mapunda.
“Utakuta baadhi ya watoa huduma wanawalazimisha wanachama wetu kuweka saini kabla ya kupata huduma huduma, tabia hii haikubaliki hata kidogo hivyo tunawaomba sana wanachama wetu mtusaidie kutupa taarifa za vituo vinavyofanya udanganyifu huu ili nasi tuweze kuwachukulia hatua stahiki,” anasema Mapunda.
Alisema kuwa ni lazima kila mwanachama atambue kuwa Mfuko huu ni mali yake na umma kwa ujumla hivyo ana wajibu wa kulinda pale anapoona unahujumiwa.
Alitumia mwanya huo kuwapongeza askari hao kwa kuonesha na kufuata taratibu zote wakati wa kupata huduma katika Vituo mbalimbali vilivyosajiliwa na Mfuko huo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya maofisa polisi Mganga Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi Mrakibu wa Polisi Dk. Hussein Yahaya aliushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuboresha Mafao na kuwa karibu na Wadau wake wakati wote.
Nae Mratibu wa Polisi Mkoa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi Richard Mollel, amewataka maofisa na askari polisi wote Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha kwamba wanajaza fomu za uanachama haraka iwezekanavyo ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza mara askari anapougua na kutaka kupata huduma.
Aidha umeuomba Uongozi wa Mfuko kuharakisha utengenezaji wa Vitambulisho ili kuondoa usumbufu pale mwanachama anapougua na kulazimika kufuata kibali katika Ofisi za Kanda.
Wakati huo, Mapunda aliwashauri askari hao na watumishi wengine kuwalipia bima ya afya ndugu na familia zao ambao hawapo katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye utaratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA) utaratibu unaomtaka mwanachama kuchangia mara moja kwa mwaka na kupata matibabu kwa kipindi chote cha mwaka.
Tuesday, June 12, 2012
Home
Unlabelled
Polisi tusaidieni kukomesha udanganyifu-NHIF
Polisi tusaidieni kukomesha udanganyifu-NHIF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment