HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 14, 2012

Gari Yawaka Moto Jijini Dar Mchana huu

 Gari ndogo aina ya Land Rover Freelander lenye nambari za usajiri T 365 ATN likiteketea kwa moto mchana huu katika barabara ya Mtaa wa Lumumba jijini Dar.chanzo cha moto huo ambao umeiteketeza kabisa gari hiyo upande wa injini ambao moto huo ulianzia bado hakijafahamika mpaka sasa.hakuna aliedhurika waka kujeruhiwa katika ajali hiyo.
 Gari ikiendelea kuwaka moto huku juhudi mbali mbali zikifanyika ili kuuzima moto huo.
Wasamalia Mbali mbali wakijitosa kusaidia kuuzima moto huo ambao ulikuwa ukiwaka kwa kasi sana.
 Sehemu ya Mabaki ya moto kutoka kwenye gari hiyo yakiendelea kuwaka huku msamalia akijaribu kuzika kwa kutumia mchanga.

 Wasamalia wakiisukuma gari hiyo ili ikae katika sehemu ambayo hakuna magari mengine wakati ikiendelea kuwaka moto kabla ya gari la zima moto kutoka manispaa ya Ilala kufika.
 Juhudi za kuuzima moto huo zikiendelea.
 Mashuhuda wakiangalia gari hiyo wakati inateketea kwa moto mchana huu,huku gari ya zima moto kutoka manispaa ya Ilala ikiwa imewasili tayari kwa kuuzima moto huo.

 Sehemu ya Injini ya Gari hiyo ikiwa imeteketea kabisa.
  Wakiisukuma ili kuitoa katikati ya Barabara.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mchana huu katika barabara ya Mtaa wa Lumunda,Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam baada kufanikiwa kuuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye gari hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad