Katibu Tawala Msaidizi(Elimu) wa Mkoa wa Tanga,Ramadhani Chomola akimkabidhi mmoja wa walimu wa michezo wa shule za Sekondari zilizopo Wilaya za Mkoa wa Tanga mara baada kuhitimu kozi ya ukocha wa mchezo wa mpira wa wavu daraja la kwanza iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Tanga Ufundi,mafunzo hayo yaliandaliwa na chama cha mpira wa wavu nchini (TAVA) kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo huo Duniani FIVB chini ya mfuko wake ujulikanao FIVB development Fund.jumal ya walimu 32 walishiriki kozi hiyo.
Walimu wa michezo wa shule za Sekondari zilizopo katika Wilaya za Mkoa wa Tanga wakiwa katika mafunzo kwa vitendo wakati wa kozi ya ukocha wa mchezo wa mpira wa wavu daraja la kwanza iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Tanga Ufundi,mafunzo hayo yaliandaliwa na chama cha mpira wa wavu nchini (TAVA) kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo huo Duniani FIVB chini ya mfuko wake ujulikanao FIVB development Fund.
WALIMU 32 wa michezo kutoka shule za Sekondari,wamefuzu rasmi kuwa makocha daraja la kwanza wa mchezo wa wavu baada ya kuhitimu mafunzo yaliyoendeshwa na Chama cha mpira wa wavu nchini TAVA kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo huo Duniani FIVB.
Walimu hao kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Wilaya zilizopo Mkoa wa Tanga,wameweza kuhitimu mafunzo hayo yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Tanga Ufundi na kuendeshwa na wakufunzi wa mchezo wa wavu wa chama cha TAVA.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyeti pamoja na vifaa vya mchezo huo kwa ajili ya shule walizotoka walimu hao,Ras wa TAVA Taifa,Augustion Agapa alisema chama chake kwa kushirikiana na FIVB kupitia mfuko wake wa maendeleo ujulikanao FIVB development Fund kiliamua kuendesha mafunzo hao ili kuhuisha mchezo huo mashuleni.
Alisema TAVA ilifanya utafiti na kubaini kwamba mchezo wa wavu umezorota kutokana na Serikali kuzuia michezo mashuleni nchini kwa kipindi kirefu na hivyo kusababisha zaidi ya miaka 8 wanafunzi kutocheza wala kufanya mashindano jambo lililosababisha walimu wengi waliopo mashuleni hivi sasa kutojua michezo.
“Tumefanya utafiti na kubaini shule nyingi hivi sasa hazina walimu wa michezo kwa sababu Serikali ilizuia kwa zaidi ya miaka nane,kwa hiyo ili kufufua mchezo wa wavu tumeamua kuendesha mradi wa kuwapa mafunzo ya mimbu za kufundisha mchezo huu walimu wa michezo mashuleni”alisema Agapa.
Alisema hadi sasa tayari mafunzo kama haya yameshafanyika Visiwani Zanzibar,Tanga na Manyara na kwamba ifikapo Septemba mwaka huu TAVA imepanga kuhakikisha mikao 12 itakuwa yatakuwa yamefanyika.
Akitoa nasaha baada ya kukabidhi vyeti pamoja na vifaa vya mchezo huo zikiwamo nyavu,mipira na vitabu vya kufundishia,Katibu Tawala Msaidizi(Elimu) wa Mkoa wa Tanga,Ramadhani Chomola aliwataka kutumia ujuzi walioupata kwa kuahikisha mchezo wa wavu unakuwa mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment