HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 3, 2012

Rais Kikwete ateua Wabunge watatu wapya leo,James Mbatia ni Mmoja wa Wabunge hao wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.

Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Mei, 2012

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad