Mchezaji wa timu ya Pool ya Chuo cha Mzumbe Morogoro, Joel Masaro akijitaalisha kupiga mpira wakati wa mashindano ya Mchezo wa Pool kwa wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendelea leo mkoani Morogoro kwa udhamini mkubwa wa Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Safari Lager. kushoto ni refa wa Mchezo huo,Prosper Nkya
Refa wa Mchezo wa Pool kwenye Mashindano ya Vyuo vya Elimu ya Juu nchini,Prosper Nkya (kushoto) akiwahesabia wachezaji wapige mpira kwa ajili ya maamuzi ya kujua nani atatakiwa kuanza kucheza na nani atafata wakati wa mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo ya Elimu ya Juu,Mkoani Morogoro leo.Mashindano hayo yanadhaminiwa na Kampuni ya bia Tanzania kupitia bia yake ya Safari Lager.
Mchezaji wa timu ya Pool ya Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA),Cleophece Cravery akipiga mpira wakati wa mashindano ya Mchezo wa Pool kwa wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu yanayoendelea leo mkoani Morogoro kwa udhamini mkubwa wa Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Safari Lager.
No comments:
Post a Comment