HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 8, 2012

Grand Malt yapanda Miti Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro leo

Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam (alieinama katikati) akipanda Mti katika Eneo la Campas ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Mazimbu Mkoani Morogoro mapema leo asubuhi wakati wa zoezi la Upandaji Miti katika eneo hilo ikiwa ni Muendelezo wa kauli ya Serikali ya kutaka kuyatunza Mazingira.Wengine pichani ni Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo hicho pamoja na Wawakilizi wa TBL Mkoani Morogoro.
Katibu Kiongozi wa Mazingira wa Campas ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Mzee Torokoko akipanda Mti katika Eneo la Chuo hicho mapema leo asubuhi.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakishirikiana na Maafisa wa TBL mkoa wa Morogoro kupanda miti mbali mbali kwenye eneo hilo.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam (kulia) akisaidiana kupanda mti na Wasimamizi wa Vituo vya Mauzo vya Jumla mikoa ya Morogoro na Dodooma,Mohamed Mbiku (kushoto) na James Gomile (pili kushoto) pamoja na Mwanafuzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),Patrick Fulanomponi.
Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) walioshiriki kikamilifu zoezi la upandaji miti katika eneo la Chuo hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad