HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 9, 2012

Fortune wa Manchester United Kuzindua Airtel Rising Stars kesho

Mchezaji nguli wa Klabu ya Manchanchester United ya Uingereza Quinton Fortune kesho atashiriki uzinduzi rasmi wa mashindano ya kuibua vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars.

Uzinduzi huo utafanyika kwenye hotel ya Sea Cliff iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technologia, Mheshimiwa Makame Mbalawa na kuhudhuriwa na chama cha mpira wa miguu TFF na waandishi wahabiri.

Mashindano ya Airtel Rising Stars yalianzishwa mwaka jana na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza yakiwa na lengo ya kuibua na kukuza vipaji vya soka nchini Tanzania.

Programu hii pia inajumuisha nchi mbali mbali za Africa kwa lengo lile lile la kusaidia maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Mwaka huu tena Airtel inaendeleza dhamira yake ya kuinua kiwango cha mpira wa miguu nchini ambapo michuano hii mikali ya kutafuta vipaji itazinduliwa rasmi kesho na Gwiji wa soka na mchezaji wa zamani kiungo wa Manchester united bwana Quinton Fortune

Hii ni nafasi ya peekee kwa vijana wetu na wapendeze wa soka kupata burudani na vijana kuonyesha vipaji vyao katika mpira wa miguu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad