HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 6, 2012

Bonanza la Ufunguzi wa Mashindano ya Excel With Grand Malt 2012 lafanyika mjini Dodoma leo

 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Kati,Nick Tesha akizungumza na wadau kutoka vyuo vyuo vya Elimu ya Juu,wakati wa Bonanza la ufunguzi wa Mashindano Excel With Grand Malt 2012 kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu,lililofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central nyuma ya Benki ya NBC,Mjini Dodoma.Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo,Consolata Adam.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano Excel With Grand Malt 2012,Consolata Adam akifafanua namna mashindano hayo yatakavyofanyika kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Mjini Dodoma leo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Joh Makini akitoa Burudani kwa wakazi wa Dodoma jioni ya leo wakati wa Bonanza la ufunguzi wa Mashindano Excel With Grand Malt 2012 kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu,lililofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central nyuma ya Benki ya NBC,Mjini Dodoma.
Joh Makini akiimba moja ya Nyimbo zake na Msanii Chipukizi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (U-Dom) jioni ya leo.
Kiduku pia kilikuwepo kutoka Dogo huyu ambaye alipanda jukwaani na kuanza kuangusha moja moja.
Wadau.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad