Ndugu zangu,
Jana amemezikwa Steven Kanumba , kipenzi cha wengi.
Mauti ya Steven Kanumba yanatukumbusha wanadamu ukweli huu; kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Hivyo, lililo jema kwetu wanadamu ni kuishi kwa kutenda yalo mema.
Kuwatendea mema hata tunaodhani wametukosea, maana, tutawasaidia kujifunza kutenda mema. Na ni mwanadamu gani asiyekosea?
Na moja ya adhabu kubwa mwanadamu unaweza kuipata humu duniani kutoka kwa wanadamu wenzako ni adhabu ya kutengwa na wanadamu wenzako.
Msichana Lulu ameshapata na anaendelea kuipata sasa, adhabu kubwa sana kutoka kwa wanajamii. Adhabu ya kupewa hukumu ya mauaji na kutengwa na wengine. Lulu , ambaye ni mmoja wa waliokuwa karibu na marehemu Kanumba hata katika dakika zake za mwisho maishani, na ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba, hakuweza kushiriki mazishi ya mpenzi wake. Hiyo nayo ni adhabu kubwa kwa Lulu kupewa na wanadamu wenzake.
Yumkini Lulu ana mapungufu yake kama mwanadamu, lakini, kwa sasa hastahili adhabu kali hiyo kutoka kwa wanajamii. Kwa kosa ambalo hakuna aliye na hakika leo kuwa amelitenda.
Ndio, Lulu aweza kuwa mwanadamu mwenye mapungufu yake mengine, lakini , hayo yasitufanye wanadamu tuwe na haraka ya kumpa hukumu isiyo ya haki. Na kwenye mienendo ya maisha, ni mwanadamu gani asiye na mapungufu?
Maana, tangu mara ile ilipofahamika, kuwa msichana Elizabeth ‘ Lulu' Michael alikuwepo kwenye mazingira ya kutokea kwa kifo cha Kanumba, basi, jamii, huku ikisaidiwa na vyombo vya habari, haraka ikapata wa kumnyoshea kidole.
Na hukumu ya Lulu kutoka kwa wanajamii walo wengi ikawa imetolewa hapo. Kwamba Lulu ndiye muuaji. Kwa sasa, hukumu hiyo haiwezi ikawa ya haki mpaka pale wenye mamlaka ya kututhibitishia hilo watakapofanya hivyo.
Na hata kama ugomvi, uliotokana na wivu wa kimapenzi , wa Lulu na mpenzi wake ulipelekea mauti ya Kanumba, bado maelezo tuliyoyasikia hayamwonyeshi Lulu kuwa na dhamira ya kutaka kutenda maovu anayohukumiwa na wanajamii kuwa kayatenda. Hivyo, naye, kama mwanadamu, anastahili msamaha kutoka kwa wanajamii wengi walo wema.
Katika wakati huu mgumu sana kwa msichana Lulu, vyombo vya habari viwe mbele katika kumsaidia Lulu kama mwanadamu mwenzetu, badala ya kutumia balaa lililomkuta kama mtaji wa kuandika na kutangaza udaku wa kuuzia magazeti na kuvutia watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio.
Maana, kwa adhamiriae kutumia magumu yanayomkabili msichana Lulu kuvuna, basi, hana atakachokivuna zaidi ya kuvuna dhambi.
Badala yake, media isaidie katika kutufanya wanajamii tujitafakari. Kwa vile, habari za matukio ya mahusiano yasiyo na staha na matendo ya kiuhuni yanayofanywa na baadhi ya wanajamii wakiwemo wasanii, huwa yanashabikiwa na vyombo vya habari badala ya vyombo hivyo kushiriki kukemea na kuelimisha jamii.
inasikitisha, kuwa katika wakati huu, vyombo hivyo vya habari vyaweza kabisa kuwa kwenye harakati za kuandaa stori zaidi za ‘ kumning’iniza’ zaidi Lulu ambaye tayari ameshaning’inizwa hadharani.
Ndugu zangu,
Kama wanajamii, na wengine kama wazazi. Lulu anabaki kuwa ni msichana mdogo anayehitaji kusaidiwa katika wakati huu mgumu kwa maisha yake. Yumkini vyombo vya dola vinaweza vimtie au visimtie hatiani. Hivyo, kumwachia huru Lulu.
Lakini, bado hukumu ya jamii ikabaki pale pale. Hukumu ya Lulu kutengwa na jamii. Hiyo ni hukumu mbaya zaidi inayoweza kuchangia hata kuyafupisha maisha ya msichana huyu mdogo. Jamii haina faida na hukumu kama hiyo.
Ni heri ikamwacha huru aende akapambane na yanayomkabili mbele yake. Ndio, akapambane na maisha haya magumu ya dunia hii bila kujisikia kutengwa na wanajamii wenzake.
Na naamini, leo kuna wengi kama mimi, wenye kufikiri hili, kuwa jamii ya walo wema imsamehe Elizabeth ‘ Lulu’ Michael.
Na hilo ni Neno La Leo.
Nilikuwa na hasira sana na Lulu lakini baada ya kusoma neno la leo kutoka kwa mdau,nimeona umuhimu wa kumsamehe na nina imani sisi wanajamii hatustahili kumhukumu. It's hard but i believe it will be fare to let nature take it's cause. Let's be patient till proven guilty.
ReplyDeleteLulu,Marehem&God ndio mashahidi wa tukio, Tusihukumu tusije hukumiwa. Hata kama mahakama itamuachia tayari psychrogicaly she have been affected. Amurudie Mungu na Roho mtakatifu atamfariji.
ReplyDeleteUnachosema ni kweli ukizingatia, ukipoteza umepoteza hata tukimhukumu Lulu haitatusaidia. Tungekua tunamkinga kabla ya kifo ingekua nzuri zaidi. Ila Ugomvi si mzuri kila watu tunatembea tumekufa na siku zote kifo kinatafuta sababu.
ReplyDeleteTunaitaji kufikiri maisha yetu zaidi baada ya kufa, kama tunaona Mwenzetu ametangulia akiwa mdogo kabisa,ni maisha gani tunayoishi if there is Life After Death... Get Ready for whatever happen now.
Nadhani perception ya Lulu kwa tabia zake zenye mikasa mingi kwene jamii ndo inapelekea yote hayo. Sidhani kama alidhamiria kuumua Kanumba kama alikua na uhusiano nae ya kimapenza labda angekua jambazi kweli ningeweza kufikiria alikua kibiashara zaidi. Nadhani tunahitaji kulipokea kama lilivo na kukubaliana na ukweli. ALTHOUGH IS HARD TO BELIEVE & IT HURTS,Epecially for the family members,Friends and Other.Ukizingatia it was the time we need him at most.
ReplyDeleteMaisha ya Kanumba yaliandikwa hivyo na yote yametimia ila Kila kifo hakikosi sababu,ndio Maana Lulu anaonekana VICTIM,Kumhukumu ama kutokumuhukumu Nothing will change from the realiality we have lost I mean we have LOST. Tusamehe sababu hamna aliye na ukweli juu ya hilo.
Mimi binafisi naungana na wewe kwa mawazo yako, lakini napenda kusema kuwa nirahisi sana kusema jambo lolote kama halitakuwa linakugusa moja kwa moja.
ReplyDeleteMwisho napenda kutoa wito kwa watanzania wote kuwa, "sisi kama wanadamu hatujui ukweli wowote juu ya jambo hili, lakini Mungu atafanya miujiza yake,kama ume uwa kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga".
mimi kama mama, naunga mkono mada na neno la leo. Naongez\a, hebu tuaangalie upande wa pili, mathlani, katika purukushani ya kuvuta ni kuvute iliotokea kwa wapenzi hawa na kupelekea mmoja wao kuanguka na kupoteza maisha, je tutafakari kama ingekuwa Lulu ndie alioanguka na kupoteza maisha, mwenzake ambae yuko mbele ya haki kwa sasa, jamii hii ingemtenga na kumhukumu kama wanvyo mtenga na kumhukumu huyu mtoto? hili ni swali, na kama itawezekana iwe maoni yangu....
ReplyDeletekifo ni kifo hasa inapotokea kwa kijana mpiganaji, wazazi wanaumiwaq sana, na jamii inayo mzunguka... tuombeane Mungu sote tuwe na subira, tungoje sheria itakavyo tuoa hukumu yake... pole kwa wote..