Na Ripota wa Globu ya Jamii.
BENDI ya Mashujaa Music imeendelea kuibomoa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambapo safari hii imewanyakua wanamuziki wake wawili ambao ni rapa Saulo John ‘Ferguson’ na mpiga tumba nguli Sudi Mohammed ‘MCD’.
Meneja wa Mashujaa Musica King Dodoo akiongea na Ripota wa Globu ya Jamii,alisema kuwa wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika ushindani wa muziki ambapo wasanii hao wamejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa upande wa wasanii hao kila mmoja alisema ameamua kujiunga na bendi hiyo
kwa ajili ya kuendel;eza kipaji alichonacho sambamba na maslahi mazuri ambayo wamepewa na watakayopewa pindi watakapokuwa wakiitumikia bendi hiyo.
“Kikubwa ni maslahi ndiyo yamenipeleka Mashujaa Musica kwani siku hizi kila mtu anaangali maslahi yake kwanza, pia nataka kuendeleza umahiri wangu katika upigaji tumba ,”Alisema MCD ambaye ameitumikia Twanga Pepeta kwa miaka 12.
Naye Ferguson tayari ametunga vibao vitatu kwa ajili ya mashabiki huku pia akitarajia kutambulisha mtindo mpya uitwao ‘Kibega’
No comments:
Post a Comment