HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 10, 2012

MAZISHI YA KANUMBA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR MCHANA WA LEO

 Kamanda Kova akiweka mambo sawa mara baada ya watu kuzidi kusogea sehemu ya kaburi,na kufanya shughuli ya mazishi kusimama kwa muda.. 
 Waziri Nchimbi akijadiliana jambo na baadhi ya wanakati ya mazishi ya marehemu Kanumba mchana huu.
 Mh. Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo pia yupo makaburini hapa kuhakikisha shughuli inakwenda sawa.
 Waombolezaji.
 ulinzi upo na ulikuwa ukijitahidi kwa kila hali kuwadhibiti watu wasisogee sehemu lilipo kaburi la Kanumba.
 kwakeli watu ni wengi sana makaburini hapa na kuna wengine ambao wanaanguka kwa kukosa hewa,ila vijana wa red cross wako makini katika hilo.
 Wanahabari nao wanapata picha kwa shida  sana maana watu ni wengi kupita kiasi makaburini hapa.
 Waombolezaji wengine wakiwasili makaburini hapo.
 Mama wa Marehemi Steven Kanumba akiwasili Makaburini hapa akiwa ameambatana na Dada Asha Baraka.
 Muda mfupi uliopita kuna watu ambao walikuwa juu ya mti namna hii na tawi la mti limekatika na kuna baadhi ya watu wameumia na kukimbizwa hospitali.na Kamanda Kova ametoa amri kwa watu wote walio juu ya Miti washuke mara moja maana wanaweza kupata madhara makubwa zaidi. 

5 comments:

  1. Mungu ailaze roho ya marehemu Kanumba mahali pema peponi. R.I.P Kanumba

    ReplyDelete
  2. Tumuombee kwa Mungu ndugu yetu, tuwe na moyo wa uvumilivu kwani sote njia yetu ni moja

    ReplyDelete
  3. Mmmmh! Kwakweli alikuwa mtu wa watu wa aina zote bila kubagua! Mungu ampumzishe kwa amani na amsamehe makosa yake yote! Aliyoyatenda kwa kujua na kwakutokujua pia! Atakumbukwa daima milele! Amen.

    ReplyDelete
  4. am kweli brog yenu ni nzuri sana nimekuwa nkifuatilia shughuli zote kwa kupitia brog yenu mugu awajaalie wote mliokuwa pamoja toka mwanz mpaka mwisho wa shughuli hiyo ya mazishi ya marehemu KANUMBA STEVEN.

    ReplyDelete
  5. nadhani Kanumba yeye amemaliza safari yake,lamuhimu hapa ni sasa na sio kanumba tena,tunatakiwa kwa kupitia kifo cha kanumba tumrudie Mungu na kujikumbusha kuwa nasi tu safarini,hatujua kesho ni zamu ya nani,so tujiandae jamani ile kama kesho itakuwa zamu yako au zamu yangu basi tuwe na huakika huko tuendapo,,RIP DA GREAT KANUMBA

    ReplyDelete

Post Bottom Ad