Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR), ulioanza jana Aprili 16, 2012 jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Mwele Malecela (watatu kushoto) kuhusu maonyesho ya wanasayansi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR) wakati alipofika kufungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa sayansi ulioanza jana Aprili 16, jijini Arusha. Wa pili (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mponda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Dennis Massue, kutoka Kituo cha Utafiti Amani Tanga kuhusu vipimo vinavyofanywa na kituo hicho kwa kupima ufanisi na ubora wa Viuatilifu vinavyoua Mbu katika Vyandarua kwa kutumia kifaa cha kupima ubora ‘Cone Bioassay’, wakati alipotembelea katika maonyesho ya wanasayansi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya magonjwa ya Binadam (NIMR) alipofungua mkutano wa 26 wa mwaka wa wadau wa sayansi ulioanza jana Aprili 16, jijini Arusha. Wa pili (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal, (katikati) ni Dkt. Mwele Malecela.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na wadau wa Sayansi waliohudhuria mkutano huo wa 26 wa mwaka wa Wadau wa Sayansi jijini Arusha jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Aprili 17, 2012. Kulia ni Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment