HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 28, 2012

Candila Bahame azindua maoenesho ya wiki mbili ya kazi zake za sanaa ya uchoraji

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama, Candida Bahame (kushoto)akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba wakati wa ufunguzi wa maonesho ya mauzo ya kazi z sanaa za Mama Bahame yanayoendelea katika Gallery hiyo iliyopo Mbuyuni njia ya Mwenge
Mkurugenzi Mtendaji wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba (wa kwanza) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) Chansa Kapaya wakiangaliwa picha zilizochorwa na mchoraji Candida Bahame.
Mkurugenzi wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba akizungumza na wageni waliojitokeza wakati wa maonesho ya picha za Candida Bahame yanaoendelea katika Ujamaa Art Gallery iliyopo eneo la Mbuyuni njia ya kuelekea Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama, Candida Bahame (kulia) akimuonesha mdau wa picha Jese Mnguto picha anazoziuza katika Gallery ya Ujamaa.

Na Mwandishi Wetu

WANAJAMII wametakiwa kutumia kazi za sanaa za mikono za wasanii wa hapa nchini katika kupamba nyumba zao ili kuongeza hamasa na maendeleo ya tasnia hiyo hapa nchini.

Wito huo ulitolewa juzi na Mdau wa sanaa za uchoraji Candida Bahame ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama wakati akizindua maoenesho ya wiki mbili ya kazi zake za sanaa.

Candida alisema kuwa wasanii wa hapa nchini wanao uwezo wa kuchora na kutengeneza picha kwa kutumia viashiria mbalimbali vya kisanii ambavyo zinapendezesha nyumba.

Alisema kuwa wanajamii wakiwa na utamaduni wa kununua kazi zao za sanaa na kuzipamba majumbani kwao watakuwa kwa kiasi kikubwa wamesaidia kukua kwa sanaakiwa kama mdau wa kazi za sanaa ya uchoraji hapa nchini.

“ Mimi naona kuwa muda umefika kwa hoteli zetu, ofisi na hata nyumba zetu watu kutumia picha za wasanii wa hapa nchini katika kupamba nyumba zao ili kuonesha kuwa wanathamini na kutambua sanaa zetu hapa nchini” alisema Candida.

Akizungumzia sanaa yake hiyo ambayo alisema kuwa alianza tangia miaka ya 1980, Candida alisema kuwa gharama ya picha zake anazipanga kulingana na muda aliotumia kuzichora pamoja na umaridadi wa picha hizo.

Alisema kuwa anatumia kipaji chake kufikisha ujumbe kwa njia ya maneno ambapo anatumia shanga kushona maneno yenye ujumbe na pia anatumia shanga kutengenezea picha.Maonesho hayo ya wiki mbili yanaendelea katika Ujamaa Art Gallery.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad