HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 26, 2012

Utaalam Uliotukuka wa Wezi wa kwenye mabegi ya watu kwenye viwanja vya ndege (Air Port)

Niliposafiri kwa mara ya kwanza nje ya nchi, nilisahau ufunguo wa sanduku nyumbani. Nilipofika kiwanja cha ndege wakati wa kukaguliwa, nilitakiwa kufungua sanduku ili kupunguza baadhi ya vitu, lakini kwa kuwa sikuwa na ufunguo, ilinilazimu ama niliache sanduku zima lirudi nyumbani au nichane na kuondoa vitu na kulisafirisha likiwa na hitilafu.

Wakati nikiwaza cha kufanya, mfanyakazi mmoja anayeshughulika na mizigo alinihurumia, akaniita pembeni, akaniuliza kama nina kalamu (bahati nzuri nilkuwa nayo), akanielekeza jinsi ya kufungua na kufunga sanduku bila kutumia ufunguo wala kuharibu kufuli. Nilifanikiwa kulifungua na kupunguza mizigo, uzito ukaenea, nikaendelea na safari.

Hivi majuzi ndugu yangu amepoteza laptop iliyoibwa kwenye sanduku alilolisafirisha. Nilijaribu kumwelezea kwenye simu jinsi wizi huu unavyofanyika, ndugu yangu hakunielewa hadi nilipommtumia video inayoonekana hapo chini.

USHAURI wa jinsi ya kuhifadhi vifaa vyako kuepuka udokozi: Unaposafiri na vitu kama vile laptop, tablet, simu, kamera, iPod, mp3 player, au kifaa chochote cha thamani kubwa lakini kinabebeka (portable) kwenye mkoba wa mkononi, tafadhali viweke vifaa hivyo kwenye mkoba huo kwani huo unahesabika kama carry-on na unaruhusiwa kuingia nao kwenye ndege (soma tiketi yako ina maelezo ya idadi na uzito wa carry-ons unazoruhusiwa kuwa nazo) na hivyo utakuwa na uhakika mara zote wa vitu vyako "kibindoni" tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.

Kama itakulazimu kuviweka vifaa hivyo ndani ya sanduku litakaloingia kama mzigo hadi mwisho wa safari ndipo ulipokee sehemu ya kuchukulia mizigo, basi hakikisha (1) Unavificha vifaa vyako ndani, katikati ya sanduku na kuweka nguo na vitu vingine juu ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kuona au kuhisi kuwa kuna kifaa kama laptop kwa maana kuacha laptop juu ikachora alama na taswira ya laptop, hii ndiyo wadokozi huiona na kushawishika kufungua na kuiba au (2) Unaingia gharama iliyopo katika baadhi ya viwanja vya ndege, ya kununua ile nailoni wanayofunga kuzunguka sanduku zima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad