HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 6, 2012

UN YAENDESHA WARSHA KWA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI YA ZANZIBAR

Waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame akifungua warsha ya maafisa mawasiliano wa Wizara husika Zanzibar. Katikati ni kaimu mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na kulia ni Mwakilishi Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alberic Kacou.
Kaimu Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Ruth Leano na naye aliwakilisha program za UN zilizopo Zanzibar.
Baadhi ya maafisa mawasiliano wakifuatilia kwa makini warsha iliyoandaliwa na UN.
Picha ya pamoja.

Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kupitia kundi la maafisa mawasiliano linalojulikana kama United Nations Communication Group (UNCG), limeendesha warsha ya siku moja mjini Zanzibar kwa maafisa mawasiliano wa serikali ya Zanzibar wanaofanya kazi katika wizara zote za Zanzibar.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na maafisa 40 wa wizara husika na ilihusu jinsi gani ya kuwawezesha wanamawasiliano wa serikali ya Zanzibar na UN kuimarisha mawasiliano yanayohusu maendeleo ya Jamii, hususan ya Zanzibar.

Mheshimiwa Dr. Mwinyihaji Makame, waziri wa nchi ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar alifungua warsha hiyo. Julai 2011, UN pamoja na serikali ya Tanzania ilisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo wa miaka minne (UNDAP).

Mpango huu umelenga kufanya kazi kwa pamoja na serikali ya Tanzania. Utoaji wa warsha kwa maafisa Mawasiliano wa serikali ni moja ya mikakati ya kuimarisha utoaji taarifa wa maendeleo ya programu zinazofanywa kwa pamoja ambapo kundi la Mawasiliano la UN litakutana na wanamawasiliano wa bara mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad