Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akihutubia leo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam leo, huku Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Frederick Sumaye wakiwa miongoni wa wageni mashuhuri walkioalikwa na kutunukiwa tuzo kwa juhudi zao zilizofanikisha kuanza na kushamiri kwa NHIF
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa Tuzo ya Kuenzi mchango wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Bima ya Afya katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo uziliofanyika kwenye ofisi kuu ya mfuko, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Machi 19, 2012.Kushoto ni Waziri Mkuu, Frederick Sumaye ambaye pia alipewe tuzo hiyo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa (katikati) na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Bima ya Afya kwenye ofisi kuu ya mfuko huo barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Mh Wilson Mukama akipokea tuzo kwa mchango wake kufanikisha utendaji wa NHIF
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akizindua kitabu cha taarifa za mfuko huo vijijini zilizokusanywa na wanahabari katika mikoa mbalimbali nchini. Kushoto ni Ofisa Habari na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael.
Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya NHIF, Profesa Lucian Msambichaka akipatiwa tuzo na Mizengo Pinda
Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Mjumbe mstaafu wa Bodi ya NHIF, Margareth Sitta akipatiwa Tuzo.
Mmiliki wa Blog maarufu ya Michuzi, Muhidin Issa Michuzi, akipatiwa tuzo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya baada ya kuwa mmoja wa mashujaa waliosaidia mfuko huo kusonga mbele.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya (kushoto) akimkabidhi tuzo maalum, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Emmanuel Humba kwa kutambua mchango wake mkubwa ikiwemo kutokata tamaa alipokuwa akishambuliwa na wadau waliokuwa wakipinga kuanzishwa kwa mfuko huo. Brass Band ya Polisi ikitumbuiza
Ankal akiwa miongoni mwa Mashujaa wa NHIF waliotunukiwa tuzo leo
Da' Faraja Kihongole wa Channel 10 akiwa na tuzo yake, akiwa na mwanahabari mwingine mkongwe Joyce Bazir ambaye pia alitunukiwa tuzo kwa kusaidia kueneza elimu kwa umma juu ya NHIF
Ankal baada ya kupokea tuzo yake |
No comments:
Post a Comment