Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Emmanuel Mhehwa(kulia) ambaye ni mlemavu wa macho juu ya namna anavyoweza kutumia kompyuta maalumu za watu wenye ulemamavu kuandika na kuhifadhi taarifa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.Taarifa za wizara ya afya na ustawi wa jamii zinaonyesha kuwa Tanzania ina watu karibu laki 450,000 wasioona na watu 1,350,000 wenye uoni hafifu. 
Waziri  wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akifurahia jambo na  mwimbaji na mpiga gitaa mahili wa Bendi ya watu wenye ulemavu (Blind  Beat Band) mzee Bonifasi Kiyenze leo jijini Dar es salaam wakati wa  hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho  nchini. Bandi hiyo ni miongoni mwa vikundi vya burudani vilivyoalikwa  kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Waziri  wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akizindua Mpango mkakati  wa taifa wa huduma za macho wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika  viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam ambapo Tanzania  imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Glaukoma duniani ambayo  imeongozwa na kauli mbiu isemayo “Usiachie Glaukoma isababishe giza  kwenye maisha Yako”.
Waziri  wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi Kaimu mganga  mkuu wa Serikali Dkt. Donarld Mpando nakala ya Mpango mkakati wa taifa  wa huduma za macho utakaoanza kutumika nchini mara baada ya kuzinduliwa  leo jijini Dar es salaam.
Waziri  wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi nakala ya  Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini mwakilishi wa  waandishi wa habari waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mkakati huo  Bi. Zaina Jongo Malongo kutoka Gazeti la Mwananchi leo jijini Dar es  salaam kufuatia umuhimu wa waandishi wa habari katika utoaji wa elimu  kwa wananchi kuhusu sera mbalimbali.
Msanii wa Muziki na Kiongozi wa Bendi ya Muziki ya Mjomba (Mjomba Band) Bw. Mrisho Mpoto (kushoto) akifikisha ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa macho na umuhimu wa kuwahi matibabu ya macho katika vituo vya afya ili kuzuia upofu leo katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam.
Vijana kutoka kikundi cha sarakasi cha Bandi ya Mjomba kikionyesha umahiri katika mitindo mbalimbali ya sarakasi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment