Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu na na wafadhili (mstari wa mbele) sambamba na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya maji Kitaifa yalifikia tamati leo na kufungwa rasmi na Rais Kikwete mapema leo jioni kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Kupokelewa na Mkurugenzi wake wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda. Pia SBL walipokea Cheti cha ushiriki wa maonesho hayo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na wageni waalikwa wakiwa ameketi jukwaa kuu
Rais Kikwete akielekea kukagua Mabanda ya maonesho ndani ya Uwanja wa Samora mapema jioni hii,ambapo Rais Jakaya Kikwete leo amefunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Mkoani Iringa. Pamoja na kuhutubia katika kilele hicho pia Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma za maji na wadau mbalimbali wa maji nchini.
Pichani ni Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi Teddy Mapunda mara baada ya kulitembelea banda hilo,ambao ndio wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo ya mwaka huu yaliyofanyika uwanja wa Samora Mjini Iringa. na pichani kati ni Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi Teddy Mapunda akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi,Mh Rais Kikwete mara baada ya kulitembelea banda hilo.
No comments:
Post a Comment