Nimepokea maswali na maoni mbalimbali baada ya kuweka hapa video yenye maelekezo ya jinsi inavyowezekana kufungua sanduku kupitia kwenye zipu bila ya kufungua kufuli.
Wapo walioripoti kuwa vitu vyao viliibwa kutoka masandukuni na makufuli yalikuwa yamefunguliwa au kuonesha dalili ya kuchokonolewa ama hayapo kabisa. Kutokana na shuhuda hizo, wengine walitoa ushauri wa kutumia aina fulani ya makufuli ambayo yamepigwa chapa ya mashirika (agency or department) yanayohusika na usafiri kwa baadhi ya nchi, mfano TSA, ATS n.k. nami nikawafahamisha, hiyo nayo si dawa muafaka kwani hata hayo nayo yanaweza kufunguliwa.
Makufuli yoyote bila kujali aina na muuneo, yaani yawe ni yale ya namba (combination locks) au ya funguo mfano Tri-Cicle, Tri-Cycle, T-lock, Diamond, au ya chapa za TSA, ATS n.k. hayo yote yanaweza kufunguliwa kirahisi.
Video zifuatazo zinaonesha jinsi ya kufungua makufuli hayo bila ya kutumia ufunguo au kujua 'combination' ya kufuli.
USHAURI: Kama nilivyoeleza kwenye ushauri wa jinsi ya kusafiri na vitu kwenye carry-ons, ikiwa umeweka vitu vya thamani katika sanduku, ama (1) lipia waranti ili chochote kikibiwa ulipwe (yapo mashirika mbalimbali yanayotoza waranti kwa kulipia gharama kiasi fulani, bofya hapa kuona mifano) au (2) ulizia kwenye kiwanja cha ndege unakoanzia safari ikiwa wanayo huduma ya kuzungushia nailoni kwenye masanduku yako.
No comments:
Post a Comment